Latest News 17 Feb 2018

News Images

PROFESA MAKAME MBARAWA AZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA MALIPO YA TIKETI KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amezindua mfumo wa ukataji tiketi za kusafiria kutoka Mwanza kwenda Visiwa vya Ukerewe ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa Kampuni ya Huduma za Meli nchini na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali


Akizungumza katika viwanja vya Kampuni ya Huduma za Meli jijini Mwanza Mhe Prof Makame Mbarawa amesema kuwa dhamira ya Serikali chini ya Rais wa awamu ya Tano Mhe Dkt John Magufuli ni kuboresha utoaji wa huduma za Kampuni ya Meli kwa wananchi kwa kuzingatia ubora na ufanisi huku akisisitiza juu ya matumizi ya teknolojia na kupongezaWakala wa Serikali mtandao kwa kubuni na kufunga mfumo huo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato sanjari na kuyataka mashirika mengineya ummaya usafirishaji kufuata utaratibu huo likiwemo lile la reli nchini TRL

‘… Chini ya mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli tumedhamiria kufufua upya Kampuni hii ya Huduma za Meli na mashirika ya usafirishaji ya Umma, Hivyo nizidi kuwaomba watu wa wakala wa serikali mtandao tusiishie tu hapa kwa Kampuni ya Huduma za Meli twendeni tukakae tuje na mfumo mwengine mpya kwa mashirika mengine …’ Alisema

Aidha Waziri huyo wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amewaasa watumishi wa Kampuni hiyo kuwa waadilifu na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakaeenda kinyume na sheria huku akiagiza kufungwa kwa kamera za usalama sehemu ya ukaguzi wa abiria kabla ya kuingia melini ili kubaini watumishi wasiokuwa waadilifu wanaoruhusu abiria wasiolipa nauli kuingia ndani ya meli hiyo

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli Bi Rose Magreth Lugembembali na kumshukuru Waziri huyo kwa kukubali na kuja kuzindua mfumo huo, amemshukuru Rais Mhe Dkt John Magufuli, Wataalamu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe John Mongela kwa namna ya kipekee katika kufuatiliashughuli za kila siku za Kampuni hiyo na kuiunga mkono ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za uboreshaji wa huduma zinazotolewa

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt Jabiri Kuwe Bakari amemuhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wakala ya serikali mtandao itaendelea kuguswa na dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kufufua mashirika na makampuni ya Umma ili yaweze kujiendeshakatika utoajiwa huduma zake kwa kusaidia mahitaji ya kimfumo kama ilivyofanya kwa kampuni ya huduma za meli ili kufikia malengo yaliyokusudiwa huku akiahidi kwenda kuongeza kipengele cha ukataji wa nauli za gharama ya mizigo inayosafirishwa katika mfumo huo

Akihitimisha Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Ndugu Eric B. Hamissi ameelezea juu ya faida zilizopatikana kwa muda mfupi mara baada ya kuanza kutumika kwa mfumo huo wa kielektroniki ikiwemo ongezeko la makusanyo ya mapato, kupungua kwa gharama za uendeshaji, udhibitiwa upotevu wa mapatona kuongezeka kwa ufanisi wa kazi huku akitaja matengenezo yaliyofanyika kwa meli ya MV Clarias na yatakayofanyika kwa meli nyengine mpya yanayotarajiwa kuanza muda si mrefu

Mhe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano alihitimisha ziara yake kwa kuitembelea na kuikagua meli ya kisasa ya Mv Clarias inayofanya safari zake kutoka Mwanza mjini kuelekea Visiwa vya Ukerewe

Imetolewa na

Kampuni ya Huduma za Meli